Mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) 2022: Yanga vs Simba

Msimu pendwa wa soka Tanzania umewadia!

Siku ya Jumamosi ya tarehe 13/08/2022 ilikutanisha mashabiki wa kandanda nchini Tanzania kufungua dimba la msimu mpya wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara, katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

 

Wana-TMC tulikua uwanjani hapo kushuhudia yanayojiri, lakini pia, tulikuwa wasimamizi rasmi wa tukio hili lililowakutanisha mahasimu wawili wa kandanda, timu za Simba na Yanga.

Hongera nyingi kwa Wanayanga kwa kuchungua ubingwa baada ya kuwachapa Simba mabao 2-1