Washindi wa mchezo wa baiskeli Tanzania wapatikana

Chama cha Baiskeli Tanzania kikishirikiana na wadau wengine wa michezo kimefanikisha tukio la kutafuta mabingwa wa uendeshaji baiskeli kitaifa lililofanyika Arusha Tanzania.

Timu ya wanaume ya Arusha A imechukua ubingwa wa jumla ikifuatiwa na Shinyanga, huku Dar es salaam ikishika nafasi ya tatu na Arusha B nafasi ya nne.

Tukio hili la siku mbili lilifanyika tarehe 29 – 30 Julai 2023 na kuhusisha mbio za aina tatu; Road Race wanaume (kilometa 147) na wanawake (kilometa 73.7), Team Time Trial wanaume (kilometa 10.5) na Individual Team Trial wanaume (kilometa 5.5) na wanawake (kilometa 4).

Waendesha baiskeli wakiwa kwenye mashindano

Madhumuni ya mashidano hayo yalikua ni kuunda timu ya taifa ya baiskeli ambayo itaiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa na kuvumbua vipaji chipukizi.

Aidha, mashindano haya yametumika kuhamasisha wananchi kutumia mchezo wa baiskeli kuimarisha afya.

Wanawake walioibuka washindi kwenye mtanange huo ni pamoja na:

  • ITT Juniours – Regina Dotto kutoka Shinyanga
  • ITT Elite – Jolene Juma kutoka Dar es salaam
  • Road Race Juniours – Genevieve Theodory kutoka Arusha
  • Road Race Elite – Mkilikili Joseph kutoka Shinyanga

Kwa upande wa wanaume, washindi ni pamoja na:

  • ITT Juniours – Frank Malick kutoka Dar es salaam
  • ITT Elite – Hassan Shariff kutoka Tanga
  • Road Race Juniours – Frank Malick kutoka Dar es salaam
  • Road Race Elite – Frank Malick kutoka Dar es salaam