Mashindano ya Mbio za Mitumbwi 2023 Yaanza Rasmi

Wakazi wa Ilemela, Mwanza na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano ya mbio za mitumbwi kwa kanda ya ziwa yaliyoanza rasmi siku ya Jumamosi, tarehe 30/09/2023.

Mashindano haya yenye kauli mbiu ya “Boresha mazingira salama kwa mama na mtoto wakati wa kujifungua” yatafanyika katika Wilaya 11 za mikoa 5 inayozungukwa na Ziwa Victoria.

Pamoja na burudani, mashindano haya yaliyoandaliwa na Chama Cha Mbio za Mitumbwi Mwanza wakishirikiana na Kampuni ya kuandaa matukio ya The Market Changer Ltd (TMC), yamelenga kukusanya vifaa vya afya ya uzazi kwa hospitali za kanda ya ziwa, kwa ajili ya kusaidia akina mama wakati wa kujifungua.