Mashindano ya mbio za mitumbwi Kanda ya Ziwa yazinduliwa
Katika jitihada za kuendeleza michezo mbalimbali nchini, Chama cha Mitumbwi mkoani Mwanza kikishirikiana na wadau wa michezo kimeandaa na kuzidua mbio za mitumbwi kwa kanda ya ziwa, siku ya Jumamosi, tarehe 9 September 2023.
Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 16 hadi Novemba 25 kwa ngazi ya Wilaya, yakifuatiwa na fainali itakayofanyika Desemba 9, 2023, katika soko la Mwaloni, mkoani Mwanza.
Jumla ya timu 60 zitashiriki katika kinyang’anyiro hicho.