Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lafanya mkutano wake mkuu wa mwaka 2022 jijini Mwanza, ukiwashirikisha wadau mbalimbali wa soka nchini Tanzania.

Mkutano huo wa mwaka wa kawaida wa 17 wa TFF ulifanyika kwenye Hoteli ya Gold Crest Mwanza, mnamo Novemba 14 2022.

Pamoja na mambo mengine, wadau wa mpira wa miguu walijadili maendeleo ya soka nchini na namna ya kuboresha mchezo huo.

Katika kuhitimisha shamra shamra za mukutano huu, wadau wa soka walipata nafasi ya kushiriki kwenye mechi ya kirafiki, ikifuatiwa na hafla ya chakula cha jioni.

Timu ya TMC ilishiriki kama wasimamizi rasmi wa tukio zima, ikiwemo kuweka chapa (branding) ya mkutano huo maeneo mbalimbali jijini Mwanza, pamoja na hoteli husika, kusimamia uwepo wa mechi ya kirafiki, na hafla ya chakula cha jioni.