Siku ya Jumatano, tarehe 31 Agosti 2022, wananchi wa Kibaha na wageni mbalimbali walishiriki kwenye uzinduzi wa kituo kipya cha afya cha Desire Charitable Hospital and Rehabilitation Center (DCHRC).
Kituo hiki chenye vifaa vya kisasa kinatoa huduma mbalimbali za afya, ikiwemo afya ya viungo pamoja na utengenezaji wa viungo bandia, kama vile miguu na mikono.
Hospitali hii ilizinduliwa na mkuu wa mkoa wa Pwani, Mh. Abubakar Kunenge, na kuhudhuriwa na wageni kadhaa, wakiwemo wawakilishi kutoka taasisi za Tanzania Exposure na Swiss Limbs ya Switzerland, ambao wamefanikisha uwepo wa kituo hicho.
Tukio hili liliambatana na upimwaji afya bure, pamoja na kujitolea kuchangia damu kwa ajili ya hospitali ya Tumbi.
Timu ya The Market Changer (TMC) ilishiriki katika tukio hili la kihistoria kama wasimamizi, ambapo ilifanya mambo kadhaa, ikiwemo:
– Mpangilio wa meza kuu – Maturubali – Mpangilio wa sehemu ya kukaa wageni waalikwa (watu 200) – Mfumo wa muziki na matangazo – Mpangilio wa sehemu tatu za upimaji afya na uchangiaji damu – Ukaribishaji wageni – Ukataji utepe